NA SOPHIA KESSY

Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Charles Mwijage amesema kuwa lengo ni kuvutia wawekezaji
na kuongeza ufanisi na kuboresha utaratibu wa sasa wa leseni za biashara na
kutoa vibali hapa nchini wakati serikali ya Tanzania ikiwa katika mchakato wa kukuza sekta ya viwanda.
Mwijage amebainisha kuwa, mpango huo
utakutanisha bodi ya wataalamu kutoka kwa wananchi pamoja na sekta binafsi ili
kuandaa mpango kazi ambao utasaidia mazingira bora ya uwekezaji.
No comments:
Post a Comment