NA SOPHIA KESSY..
Shamba hili la
kilimo cha bamia liko pembezoni mwa barabara ya Tanga horohoro eneo la Kisosora kata ya nguvumali jijini
Tanga likiwa na ukubwa wa hekari tano, hapa ndipo wakulima hawa wadogo
wanapoendesha kilimo kwa kukodi ardhi kwa msimu.
Licha ya juhudi kubwa za wakulima hawa, changamoto yao
kubwa ni ukosefu wa mbegu bora, upatikanaji wa wataalamu na soko la uhakika
litakalowaondoa katika hali ya utegemezi.
Ili kupaza sauti zao IBER inafika katika eneo
hilo na kuzungumza na Bibi AZINATI HIYOBU , AMINA BAKARI na FADHILUNA YAHAYA ambao licha
ya umri wao mkubwa ndoto zao ni kuondokana na jembe la mkono.
Akijibu hoja hiyo Afisa Kilimo Kata ya Mafisa Mkoani humo
amesema amewataka wakulima kubadilika na
kuachana na kilimo cha mazoea na badala
yake watumie elimu kutoka kwa wataalam kujiendeleza.
Ili wakulima hawa kuweza kutimiza ndoto zao ni vema
taasisi za kifedha kupunguza masharti ya mikopo ili wajasiriamali hawa waweze
kukopesheka na kujinunulia pembejeo zao wenyewe.
No comments:
Post a Comment