Sunday 13 November 2016

AIRTELL YATOA ZANA KUSAIDIA WAKULIMA MISUNGWI

NA SOPHIA KESSY


Kilimo kinaajiri asilimia 80 ya wananchi nchini, licha ya idadi hiyo imebainika kuwa asilimia kumi tu ya wakulima ndio wanaoendesha kilimo chao kwa kufuata kanuni bora jambo linalosababisha wengi kupata  mazao yasiyolingana na ukubwa wa shamba.


Mkulima wa mboga mboga na Nyanya INNOCENT KIPONDYA wa Mwalogwabagole Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza, anasema baada ya Airtel FURSA kumshika mkono kwa kumpa zana za kilimo ameweza kuongeza ukubwa wa shamba na kuajiri vijana wengine.

INNOCENT amesema fursa zinazotolewa na mtandao wa Airtel, hazitolewi na mtandao mwingine nchini ambapo anatoa wito kwa jamii kuchangamkia fursa hiyo itakayobadilisha maisha yao.
 
Mradi wa Airtel Fursa umeanzishwa Mei mwaka jana na tayari umewafikia vijana zaidi ya Elfu tano katika  mikoa kumi nchini ikiwa ni pamoja na vijana zaidi ya 100 waliowezeshwa kwa kupewa mitaji.

No comments:

Post a Comment