Sunday, 20 November 2016

WAKULIMA WA VIAZI MVIRINGO WALIA NA RUMBESA




NA HAWA MOHAMED NA TULINKISA NDELWA.
 IRINGA .
 
Viazi ni miongoni mwa mazao ya chakula na biashara, zao hili kwa namna moja au nyingine hulimwa kwa lengo la kuboresha hali ya uchumi wa mkulima, kwani sasa wakulima wengi wanaendesha shughuli hii ya Kilimo cha Viazi na mazao mengine kwa ajili ya biashara zaidi,  ili kuwawezesha kumudu  kununua zana bora za kisasa –  na kuleta tija katika sekta hiyo ya kilimo.

Wakulima hawa wa zao la viazi kutoka katika kijiji cha Ihemi , Wilaya ya Iringa- wanaona gharama na nguvu wanazotumia katika kuendesha shughuli hii ya kilimo cha Viazi haiwiani  na mauzo, na tatizo kuu wakisema kuwa ni ujazo wa Lumbesa, unaochagiwa na changamoto ya kukosekana kwa Soko la uhakika na kupelekea wakulima kufuata masharti ya wanunuzi.
wakulima wengi wamejikuta wakilazimika kuuza mazao yao kwa wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya mkoa lakini hata hivyo wamekuwa wakiuza mazao yao kwa ujazo usiotakiwa kisheria, yaani lumbesa ambao umewasababishia hasara.


Jitihada za wakulima kumaliza tatizo la lumbesa bado liko chini,kwasababu ya kutokuwa na umoja wa wakuliuma hali inayopelekea kushindwa kupaza sauti yao. mbali na hiyo sababu nyingine ni wengi nwao huwa na mitaji midogo hivyo huuza kwa hasara ili mradi tu wapate pesa ya kujikimu.hivyo hulazimika kumsikiliza mnunuzi ili apate fedha ya haraka.

Tanzania Chamber of commerce, industry and Agriculture kwa kifupi TCCIA ni wadau wa Kilimo, biashara na Viwanda Tanzania. Hapa Iringa wao wamekua ni watetezi wa wakulima katika changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili.Kwa awamu tofauti tangu mwaka 2005, TCCIA  Mkoa wa Iringa wamekuwa wakifuatilia matumizi ya sheria ya lumbesa  na mwaka 2013 wametoa mapendekezo ya kuboresha sheria hiyo ili iwe na nguvu zaidi na kumkomboa mkulima.


JAMES SIZYA ni  Afisa mtendaji wa TCCIA mkoa wa Iringa yeye alisema licha ya jitihada kubwa wanazozifanya katika kumaliza tatizo la lumbesa,bado wanakumbana na changamoto kwa kuwa ni mikoa miwili tu ambayo ni irnga na njombe, imeweza kulipigia kelele tatizo hilo. hivyo endapo kutakuwa na nguvu ya pamoja kwa mikoa yote katika kukemea tatizo la lumbesa ni dhahiri linaweza kumalizika. lakini pia sizya amewasihi wakulima kujiunga katika vikundi ili waweze kuwa na nguvu ya pamoja katika kutatua changamoto zao ikiwemo changamoto ya lumbesa.

akizungumza na iber,KATIBU TAWALA MSAIDIZI wa uchumi na uzalishaji mkoa wa Iringa FIKIRA KISSIMBA alisema mikakati ya serikali kuhusiana kero ya lumbesa kwa wakulima ni kuitilia mkazo sheria ya lumbesa iweze kutumika ipasavyo, na kuifanya bkampeni ya kutokomeza ujazo usiotambulika kisheria yaani lumbesa kuwa ni ya kitaifa, ikiwa na pamoja na kuzungumza na wadau mbalimbali wa kilimo wakiwemo TCCIA na kuangalia kwa namna gani sheria inaweza kufuatwa kwa mikoa yote. 
ili changamoto ya lumbesa iishe kabisa ni jukumu la wakulima kuungana katika vikundi ili kuwa na sauti moja katika kukabiliana na changamoto zinazo rudisha nyuma jitihada zao katika kilimo biashara. na hatimaye mkulima akaweza kunufaika na kazi ya mikono yao.  

No comments:

Post a Comment