Sunday, 20 November 2016

TANZANIA YAZINDUA MAGEUZI YA LESENI ZA BIASHARA




NA SOPHIA KESSY

Serikali ya Tanzania imezindua mpango wa mageuzi ya leseni za biashara ili kuwarahisishia wawekezaji kupata huduma zenye ufanisi kwa haraka zaidi nchini humo. 

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji  Charles Mwijage amesema kuwa lengo ni kuvutia wawekezaji na kuongeza ufanisi na kuboresha utaratibu wa sasa wa leseni za biashara na kutoa vibali hapa nchini wakati serikali ya Tanzania ikiwa katika mchakato wa kukuza sekta ya viwanda. 

Mwijage amebainisha kuwa, mpango huo utakutanisha bodi ya wataalamu kutoka kwa wananchi pamoja na sekta binafsi ili kuandaa mpango kazi ambao utasaidia mazingira bora ya uwekezaji.

WAKULIMA WA VIAZI MVIRINGO WALIA NA RUMBESA




NA HAWA MOHAMED NA TULINKISA NDELWA.
 IRINGA .
 
Viazi ni miongoni mwa mazao ya chakula na biashara, zao hili kwa namna moja au nyingine hulimwa kwa lengo la kuboresha hali ya uchumi wa mkulima, kwani sasa wakulima wengi wanaendesha shughuli hii ya Kilimo cha Viazi na mazao mengine kwa ajili ya biashara zaidi,  ili kuwawezesha kumudu  kununua zana bora za kisasa –  na kuleta tija katika sekta hiyo ya kilimo.

Wakulima hawa wa zao la viazi kutoka katika kijiji cha Ihemi , Wilaya ya Iringa- wanaona gharama na nguvu wanazotumia katika kuendesha shughuli hii ya kilimo cha Viazi haiwiani  na mauzo, na tatizo kuu wakisema kuwa ni ujazo wa Lumbesa, unaochagiwa na changamoto ya kukosekana kwa Soko la uhakika na kupelekea wakulima kufuata masharti ya wanunuzi.
wakulima wengi wamejikuta wakilazimika kuuza mazao yao kwa wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya mkoa lakini hata hivyo wamekuwa wakiuza mazao yao kwa ujazo usiotakiwa kisheria, yaani lumbesa ambao umewasababishia hasara.


Jitihada za wakulima kumaliza tatizo la lumbesa bado liko chini,kwasababu ya kutokuwa na umoja wa wakuliuma hali inayopelekea kushindwa kupaza sauti yao. mbali na hiyo sababu nyingine ni wengi nwao huwa na mitaji midogo hivyo huuza kwa hasara ili mradi tu wapate pesa ya kujikimu.hivyo hulazimika kumsikiliza mnunuzi ili apate fedha ya haraka.

Tanzania Chamber of commerce, industry and Agriculture kwa kifupi TCCIA ni wadau wa Kilimo, biashara na Viwanda Tanzania. Hapa Iringa wao wamekua ni watetezi wa wakulima katika changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili.Kwa awamu tofauti tangu mwaka 2005, TCCIA  Mkoa wa Iringa wamekuwa wakifuatilia matumizi ya sheria ya lumbesa  na mwaka 2013 wametoa mapendekezo ya kuboresha sheria hiyo ili iwe na nguvu zaidi na kumkomboa mkulima.


JAMES SIZYA ni  Afisa mtendaji wa TCCIA mkoa wa Iringa yeye alisema licha ya jitihada kubwa wanazozifanya katika kumaliza tatizo la lumbesa,bado wanakumbana na changamoto kwa kuwa ni mikoa miwili tu ambayo ni irnga na njombe, imeweza kulipigia kelele tatizo hilo. hivyo endapo kutakuwa na nguvu ya pamoja kwa mikoa yote katika kukemea tatizo la lumbesa ni dhahiri linaweza kumalizika. lakini pia sizya amewasihi wakulima kujiunga katika vikundi ili waweze kuwa na nguvu ya pamoja katika kutatua changamoto zao ikiwemo changamoto ya lumbesa.

akizungumza na iber,KATIBU TAWALA MSAIDIZI wa uchumi na uzalishaji mkoa wa Iringa FIKIRA KISSIMBA alisema mikakati ya serikali kuhusiana kero ya lumbesa kwa wakulima ni kuitilia mkazo sheria ya lumbesa iweze kutumika ipasavyo, na kuifanya bkampeni ya kutokomeza ujazo usiotambulika kisheria yaani lumbesa kuwa ni ya kitaifa, ikiwa na pamoja na kuzungumza na wadau mbalimbali wa kilimo wakiwemo TCCIA na kuangalia kwa namna gani sheria inaweza kufuatwa kwa mikoa yote. 
ili changamoto ya lumbesa iishe kabisa ni jukumu la wakulima kuungana katika vikundi ili kuwa na sauti moja katika kukabiliana na changamoto zinazo rudisha nyuma jitihada zao katika kilimo biashara. na hatimaye mkulima akaweza kunufaika na kazi ya mikono yao.  

SOKO LA PILIPILI MBUZI




Na Hawa Mohamed na Tulinkisa Ndelwa  

      
Kijiji cha Luganga katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini kina wakulima wengi wa pilipili, Wakulima hao wanakabiliwa na changamoto kadhaa katika kuwa na soko la uhakika la zao la pilipili mbuzi. 

Changamoto moja inatokana na ulimbukeni wa kukurupuka kulima pilipili kwa wingi kwa kutarajia kuwa bei nzuri ya msimu uliopita ndiyo itakuwa bei ya msimu unaofuata. Wakulima hao wamejikuta wakiingia katika mkumbo wa kuchangamkia kilimo cha pilipili mbuzi kutokana na msimu mzuri uliopita.Wakulima wengi hubabaika na hulima wakiangalia zao lenye bei nzuri na pindi bei inapoporomoka na kuwatia hasara wakulima hao huamua kuachana na pilipili mbuzi kabisa.

Mbali na hasara inayoweza kumkuta mkulima kwa kulima kwa wingi kwa matarajio ya bei kubwa na hivyo kuchangia mavuno kufurika na kuharibu bei, wakulima pia hukabiliwa na kutofahamu yaliko masoko ya bidhaa yao na hivyo kulazimika kutegemea wafanyabiashara wa kati – madalali. Madalali hao hununua pilipili mbuzi kwa bei ndogo kutoka kwa wakulima na kisha kuiuza kwa wafanyabiashara wengine kwa bei kubwa.

Mkulima YOHANES JUMANNE katika kijiji cha luganga, aliongea na IBER akasema alijiikuta anashindwa kung'ang'ania bei ambayo ni kinyume na matakwa ya madalili. Aisema moja ya vitu vinavyomfanya akose nguvu ya kudai bei bora zaidi ni kwamba soko linakuwa limefurika kiasi cha kuwafanya wakulima wengine kuachana kabisa na kilimo cha pilipili mbuzi. Aliongezea na kusema ufumbuzi unaweza kuwa eneo ambalo linatambulika wazi kuwa ni soko la pilipili mbuzi.

Kuwepo kwa soko la kudumu ni kitu ambacho kinaweza kumsaidia mkulima kupata kipato zaidi. Bei ya mazao inakuwa ni yakueleweka kwa kuwa hakutakuwa na madalali, wakulima watapata fursa ya kujiendesha wenyewe pia inaongeza ujuzi na maarifa juu ya soko na biashara kutokana na uwepo wa wataalamu juu ya masoko.

FIKIRA KISSIMBA ni Katibu Tawala Msaidizi, Uchumi na Uzalishaji, mkoa wa Iringa. Yeye alisema wakulima wasioweza kupata wateja wa mazao yao kwa haraka wanapaswa kuwa na eneo ambako ndio pekee pauziwe mazao yao.


Mindombinu ya uzalishaji, usafirishaji, uhifadhi na usindikaji ni muhimu katika kuimarisha uhakika wa masoko ya mazao ya kilimo. Japo bado kuna changamoto ya uelewa mdogo kwa wakulima. Licha ya kuwepo vikundi mbalimbali vya wakulima, bado ni wakulima hawajajiunga kwenye vikundi hivyo huathiri utendaji wa wataalamu wa kilimo. Jambo hili pia huchangia kukosekana kwa taarifa muhimu ikiwemo namna ya kukabiliana na changamoto zinazowakumba wakulima. Lakini wakulima wanapojiunga katika vikundi huku kila mmoja akiwa na mawazo tofauti na mwenzake, hupelekea kushindwa kuafikiana. Kumbe, kama anavyoeleza Katibu Tawala Fikira Kissimba, vikundi vyenye maafikiano vinaweza kusaidiwa mbinu mbalimbali zinaoweza kukabiliana na kufurika kwa soko, ikiwa ni pamoja na usindikaji wa mavuno ya ziada.

Faida ya wakulima kuwa kwenye vikundi inakwenda mbali zaidi kuliko kuwapa nguvu kwenye soko. Kuwa pamoja kunaisaidia serikali au wadau wengine kuwafikia wakulima kwa urahisi ili kutoa usaidizi wa kitaalamu wa kuboresha zao lao.

Nae Afisa Kilimo kata ya Ilolo Mpya, BWANA PETER SHAYO, alisema serikali inaweza kuwa na usaidizi mzuri kwa wakulima iwapo watalima pamoja katika vikundi. Anasema hilo linaweza kusaidia hata kwenye upatikanaji wa madawa.

Matokeo ya piilipili  kufurika katika soko hupelekea kuingia kwa madalali ambao wanawanyonya wakulima kwa kuwabana kwenye bei ya shambani.

Nini kifanyike?
Kutengwa  maeneo mahususi kwa uuzaji na ununuaji wa pilipili kutawapa wakulima uhakika wa soko na kujikinga na madalali wanaowanyonya. Nguvu ya wakulima pia inaongezeka kwa kuwa kwenye vikundi na hivyo kutohitaji madalali, kwa kuwa pia wanaweza kusaidiwa mikopo, madawa na ushauri na wadau wasiowanyonya. Na pia wakulima kupatiwa ustadi wa kusindika mavuno ya ziada.

Mzigo wa kuboresha soko kwa zao lao hilo, kwa sehemu kubwa limo mikononi mwa wakulima wenyewe. Wawe na ushirikiano ili wawe na nguvu na pia waweze kupata usaidizi.

Sunday, 13 November 2016

WAKULIMA WA BAMIA MKOANI TANGA WAOMBA KUWEZESHWA



NA SOPHIA KESSY..


Shamba hili la  kilimo cha bamia liko pembezoni mwa barabara ya Tanga horohoro  eneo la Kisosora kata ya nguvumali jijini Tanga likiwa na ukubwa wa hekari tano, hapa ndipo wakulima hawa wadogo wanapoendesha kilimo kwa kukodi ardhi kwa msimu.

Licha ya juhudi kubwa za wakulima hawa, changamoto yao kubwa ni ukosefu wa mbegu bora, upatikanaji wa wataalamu na soko la uhakika litakalowaondoa katika hali ya utegemezi.

Ili kupaza sauti zao IBER inafika katika eneo hilo na kuzungumza na Bibi AZINATI HIYOBU  , AMINA BAKARI na FADHILUNA YAHAYA ambao licha ya umri wao mkubwa ndoto zao ni kuondokana na jembe la mkono.

Akijibu hoja hiyo Afisa Kilimo Kata ya Mafisa Mkoani humo amesema  amewataka wakulima kubadilika na kuachana na kilimo cha mazoea  na badala yake watumie elimu kutoka kwa wataalam kujiendeleza.

Ili wakulima hawa kuweza kutimiza ndoto zao ni vema taasisi za kifedha kupunguza masharti ya mikopo ili wajasiriamali hawa waweze kukopesheka na kujinunulia pembejeo zao wenyewe.

AIRTELL YATOA ZANA KUSAIDIA WAKULIMA MISUNGWI

NA SOPHIA KESSY


Kilimo kinaajiri asilimia 80 ya wananchi nchini, licha ya idadi hiyo imebainika kuwa asilimia kumi tu ya wakulima ndio wanaoendesha kilimo chao kwa kufuata kanuni bora jambo linalosababisha wengi kupata  mazao yasiyolingana na ukubwa wa shamba.


Mkulima wa mboga mboga na Nyanya INNOCENT KIPONDYA wa Mwalogwabagole Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza, anasema baada ya Airtel FURSA kumshika mkono kwa kumpa zana za kilimo ameweza kuongeza ukubwa wa shamba na kuajiri vijana wengine.

INNOCENT amesema fursa zinazotolewa na mtandao wa Airtel, hazitolewi na mtandao mwingine nchini ambapo anatoa wito kwa jamii kuchangamkia fursa hiyo itakayobadilisha maisha yao.
 
Mradi wa Airtel Fursa umeanzishwa Mei mwaka jana na tayari umewafikia vijana zaidi ya Elfu tano katika  mikoa kumi nchini ikiwa ni pamoja na vijana zaidi ya 100 waliowezeshwa kwa kupewa mitaji.