Thursday 19 January 2017

WANANCHI WA MKOA WA IRINGA KUNUFAIKA NA KILIMO CHA ZAO LA PARETO
Na Tulinkisa Ndelwa na Hawa Mohamed
Diwani wa viti maalum akiongea na wananchi wa Bomalang'ombe.

Mwakilishi kutoka kiwanda cha pareto Tanzania (PCT) Godfrey Mbeyela akiwaeleza wananchi wa Bomalang'ombe faida za kilimo cha pareto


Vitalu vya miche ya pareto

Wananchi wa kata wa Idete wakiwa katika mkutano wa hadhara wa uhamasishaji wa kilimo cha zao la pareto
WAKULIMA wa wilaya ya Kilolo na Mufindi mkoani Iringa wanatarajia  kunufaika na kilimo cha zao la pareto baada ya kiwanda cha Pyrethrum company Tanzania Ltd (PCT) Mafinga kuanza kugawa bure miche ya zao la Pareto .

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa uhamasishaji wa kilimo cha zao La Pareto kata ya Bomalang'ombe na Idete mwakilishi wa kiwanda cha PCT Godfrey Mbeyela, alisema kampuni hiyo imeamua kutoa miche bure ili kuwaondolea usumbufu wananchi wa kupata miche.

"Kwa mwaka huu miche ipo ya kutosha ya kuwawezesha wananchi zaidi ya 40,000 kulima Pareto ila kwa kuwa idadi ya wakulima inaweza ongezeka zaidi mwakani vikundi vitapewa kazi ya kuotesha miche na kuuza kwa kampuni….. kampuni haitaki mkulima wa zao la Pareto kununua miche"alisema Mbeyela

Na kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah aliwataka wananchi kujiunga na kilimo hicho kwani ni moja kati ya mazao ambayo hayahitaji gharama kubwa ya kuhudumia zaidi ya palizi pekee.Hivyo alishauri kila mwananchi kulima japo ekari moja ya Pareto.

Awali wananchi wa Wilaya ya mufindi walisema kuwa waliacha kulima pareto na kufyeka mashamba kisha kupanda viazi baada ya kuyumba kwa soko la Pareto.

1 comment: